WA NNE MBARONI TUKIO LA MAUAJI YA TEMBA


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne wanaohusishwa na tukio la mauaji ya James Rogers Temba, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). 

Watuhumiwa waliotiwa mbaroni ni Steven Rogers Chaka (31), ambaye ni Afisa Maabara na mkazi wa Bomang’ombe Hai, Kilimanjaro, pamoja na Anna Frank Lema maarufu kama Happines (30), mfanyabiashara na mkazi wa Tabata Chang’ombe. Wengine ni Twalibu Khamis maarufu kama Mputo (23) na Michael John maarufu kama Tambali (26), wote wakiwa ni wakazi wa Kigogo Kati jijini Dar es Salaam.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunafuatia upelelezi wa kina wa tukio la kusikitisha ambapo mwili wa James Rogers Temba ulipatikana ukiwa unaelea kwenye maji katika mto Msimbazi, eneo la Kipawa Ilala, tarehe 30 Aprili 2026 ukiwa hauna kichwa. 

Mbali na kuwashikilia watuhumiwa hao, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa linaendelea kuchunguza baadhi ya vielelezo vilivyopatikana kuhusiana na mauaji hayo. 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ametoa wito kwa wananchi kuwa watulivu wakati taratibu za kisheria zikiendelea, akisisitiza kuwa kila mhusika atachukuliwa hatua kali kulingana na ushahidi utakaopatikana.

BOSS TV

Hii ni Official blog ya BOSS MEDIA kwa habari za siasa, jamii, elimu, burudani na michezo tufuatilie kwa uhakika zaidi

Post a Comment

Previous Post Next Post