Read more
Umoja wa Waendesha Magari ya Biashara (Kirikuu) wa Manzese, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, umewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani ili kuhakikisha shughuli za kiuchumi na kijamii zinaendelea kufanyika kwa utulivu na maendeleo.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam, madereva hao wamesema amani ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa, hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuilinda, kuiendeleza na kuienzi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Aidha, wamewaomba vijana kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuvuruga utulivu wa nchi, wakisisitiza kuwa amani ndiyo nguzo kuu ya ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na kuboresha maisha ya wananchi.
Madereva hao wameeleza kuwa mazingira ya amani na utulivu huwezesha wananchi kufanya shughuli zao za uzalishaji kwa uhuru na kuchangia maendeleo ya taifa.


.jpg)
0 Reviews