Read more
MBUNGE wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, ameweka msimamo mkali Bungeni jijini Dodoma
akiwataka viongozi wanaotoa matamko yanayozua taharuki na mifarakano kuondolewa kwenye
nafasi zao mara moja, akisisitiza kuwa hawafai kuendelea kushika nyadhifa za uongozi.
Akichangia Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka
2026/27, Waitara amesema haiwezekani baadhi ya watu “kutoboa mtumbwi” huku wengine wakikaa
kimya bila kuchukua hatua za kinidhamu.
Amesema kauli na matendo ya viongozi yanapaswa kulinda umoja wa taifa badala ya kuchochea
mgawanyiko au hofu miongoni mwa wananchi.
Aidha, amewataka Wabunge na viongozi wa ngazi mbalimbali kuheshimu wananchi na kuchunga
maneno yao ili kuepuka kuibua taharuki isiyo ya lazima na kudumisha mshikamano wa kitaifa.



0 Reviews