Read more
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ndele Mwaselela, ametia wito
kwa Kanisa kuendelea kuwa nguzo muhimu ya kuhubiri amani, mshikamano na
upendo katika jamii ili kuimarisha umoja wa wananchi na maendeleo ya
Taifa.
Mwaselela
ametoa kauli hiyo leo Juni 7, 2026 katika KKKT Usharika wa Forest,
jijini Mbeya, wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya huduma ya Kwaya Kuu
Kongwe ndani ya kanisa hilo.
Akizungumza
na waumini na viongozi wa dini, amesema kumtegemea Mungu kunamjenga
mwanadamu kuwa na matumaini, maadili mema na mwelekeo sahihi wa maisha,
hali inayochangia ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla.
"Jamii
inayojengwa katika misingi ya upendo, mshikamano na kuheshimiana
huendelea kuwa na utulivu na uwezo mkubwa wa kushirikiana katika kutatua
changamoto mbalimbali," amesema Mwaselela.
Aidha,
amewahimiza viongozi wa dini na wazazi kuendelea kuwalea watoto katika
maadili mema, hofu ya Mungu na uzalendo ili kujenga kizazi chenye
nidhamu na uwajibikaji.
Pia
amewataka waumini na Watanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili aendelee
kupata afya njema na hekima katika kuwatumikia wananchi na kuiongoza
nchi kuelekea maendeleo zaidi.



0 Reviews