Read more
Katika
jitihada za kuimarisha chachu ya maendeleo nchini, Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Seneti Mkoa wa Mwanza umeandaa Kongamano la
Wasomi lililofanyika leo, Juni 7, 2026, katika Chuo cha Uvuvi Nyegezi,
likiwa na lengo la kuwajengea vijana uelewa kuhusu umuhimu wa amani,
umoja na mshikamano uliopo nchini.
Akizungumza
katika kongamano hilo, Mwenyekiti wa Vyuo na Vyuo Vikuu wa UVCCM Seneti
Mkoa wa Mwanza, Kenneth Geremia, amewasisitiza vijana kuonyesha mapenzi
ya dhati kwa taifa kwa kulinda amani, umoja na utulivu uliopo nchini.
Amesema
vijana ndio wenye kuamua hatma ya taifa, hivyo kila mmoja ana wajibu wa
kudumisha amani, umoja na mshikamano ili kuhakikisha maendeleo endelevu
yanaendelea kupatikana.
“Ninapenda
kutoa wito kwa kila kijana kufanya uwajibikaji na uzalendo kuwa
vipaumbele vyao vya kwanza katika ujenzi wa taifa, kwani vijana ndio uti
wa mgongo wa maendeleo ya nchi,” alisema Geremia.
Aidha,
amewahimiza vijana kujitolea kikamilifu katika shughuli za kijamii na
kisiasa, akibainisha kuwa uwajibikaji thabiti ni msingi muhimu wa
mafanikio ya taifa. Amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kuwa chachu ya
maendeleo badala ya kutumiwa kama nyenzo za kuvuruga amani na utulivu
uliopo nchini.



0 Reviews