MPUNJA: VIJANA WALINDE AMANI KWA AJILI YA MAENDELEO YA TAIFA

MPUNJA: VIJANA WALINDE AMANI KWA AJILI YA MAENDELEO YA TAIFA

Size
Price:

Read more


MJUMBE wa Kamati ya Uratibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Chuo Kikuu cha Kampala, Salum Mpunja, amewataka Watanzania kuendelea kuilinda na kuitunza amani ya nchi ili kuweka mazingira bora ya maendeleo na ustawi wa wananchi.

Mpunja ametoa wito huo jijini Dodoma akieleza kuwa amani ni moja ya hazina kubwa ambayo Tanzania imeendelea kujivunia kwa miaka mingi na kwamba kila mwananchi ana wajibu wa kuilinda.

Amesema mataifa mengi duniani yameathirika kutokana na migogoro na machafuko, jambo ambalo limekwamisha maendeleo ya wananchi wake. Hata hivyo, Tanzania imeendelea kuwa mfano mzuri kutokana na utulivu uliopo.

Kwa mujibu wa Mpunja, maendeleo ya uchumi yanategemea kwa kiwango kikubwa uwepo wa mazingira salama na yenye amani ambayo yanawapa wananchi nafasi ya kufanya shughuli zao bila hofu.

“Kitu ambacho napenda sana kuwasisitiza ni katika jambo la kutunza amani ya nchi yetu. Tunavyotunza amani ya nchi yetu, ndio tunaelekea nchi yetu kuwa na maendeleo makubwa,” amesema.

Ameeleza kuwa vijana ni miongoni mwa makundi yanayonufaika zaidi pale nchi inapokuwa na amani, kwani hupata nafasi ya kufanya biashara, kuanzisha miradi mbalimbali na kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali.

Mpunja amesema kuwa mazingira ya utulivu huwavutia pia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, hali inayochochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.

Aidha, amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa njia chanya kwa kueneza ujumbe wa umoja, mshikamano na uzalendo badala ya kusambaza taarifa zinazoweza kuleta migawanyiko katika jamii.

Amesisitiza kuwa jukumu la kulinda amani halipaswi kuachwa kwa viongozi pekee, bali kila Mtanzania anapaswa kuwa sehemu ya juhudi hizo kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya taifa.

Mpunja ameongeza kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kufikia maendeleo makubwa zaidi ikiwa wananchi wataendelea kuthamini amani na kushirikiana katika kujenga taifa lenye umoja, utulivu na ustawi kwa wote.

0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *