Read more
HADIA KHAMIS na ANGELINA MAGANGA, DAR
NABII wa Kanisa la WRM, Nickolas Suguye amewataka waandishi wa habari pamoja na viongozi wa dini kuhamasisha vitendo vya maadili ili kurudisha jamii katika maadili ya Mtanzania.
Ushauri huo ameutoa leo, Machi 27 Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema Kanisa limefanya mengi ikiwemo kusaidia wajane, wazee na watoto yatima pia wamefanya juhudi mbalimbali katika kuboresha miundombinu ya barabara na sekta ya afya.
Suguye amesema Aprili 1 mwaka huu Kanisa la WRM litaadhimisha miaka 17 tangu kuandhishwa kwake.
"Tarehe hiyo ni siku kubwa mno kwetu, tulimwalika Rais Dkt Samia Suluhu Hassan lakini kutokana na mwingiliano wa ratiba amemuagiza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa ndiye atamwakilisha nafasi ya ugeni rasmi," amesema Suguye.
Suguye amesema katika maadhimisho hayo kutakuwa na usafiri wa bure, chakula na vinywaji huku ikipambwa na waimbaji wa nyimbo za injili, vikundi vya kwaya, huduma za maombi na maombezi.
"Mara baada ya tukio hilo muendelezo wa kuwasaidia yatima na wajane itaendelea kwani tumejijengea utamaduni huo".
"Katika maadhimisho yetu ya miaka 17 maombezi hayawezi kuepukika siku hiyo pia wenye shida mbalimbali za kiroho wataombewa na kufunguliwa katika maisha yao" Amesema Nabii Suguye.
Aidha katika maadhimisho hayo ya miaka 17 watu mbalimbali ikiwemo Manabii kutoka makanisa mengine,wachungaji,wanasiasa na makundi mengi Mbalimbali.



0 Reviews