BENKI YA ACB, YAFUTURISHA DAR

BENKI YA ACB, YAFUTURISHA DAR

Size
Price:

Read more



Na HADIA KHAMIS, BOSS TV

AKIBA Commercial Bank (ACB) imewafuturisha wateja, wafanyakazi na wadau mbali mbali wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu yao ya kila mwaka inayowaleta karibu wateja na benki hiyo.

Akizungumza katika hafla ya futari iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa ACB Silvest Arumasi amewapongeza Waislamu wote kwa mfungo.

Arumasi amewashukuru wadau wote kwa kutenga muda wao na kujumuika pamoja katika futari hiyo kwani kitendo hicho kimeleta faraja na heshima kubwa kwao.

Aidha, amesema, ACB imekuwa na utamaduni wa kufanya hafla ya kufuturisha kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono Waislam katika funga yao na pia ni njia nzuri ya kuboresha mahusiano ya benki na wateja wake. 

"Akiba Commercial Bank inatambua na kuheshimu sana Imani za wateja, Wafanyakazi na wadau wake na inaupa umuhimu wa kipekee mwezi Mtukufu wa Ramadhan," amesema Arumasi.

Arumasi amesema kuwa ACB inaendelea kuboresha na kupanua wigo wa huduma zake ili kuendana na soko kwa lengo ya kukidhi matarajio ya wateja.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wateja na umma kwa ujumla kuendelea kuiamini Benki hiyo ambayo inawahudumia Watanzania wengi huku ikisaidia maendeleo makubwa kwa wajasiriamali na Jamii nzima kwa ujumla.

0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *