Read more
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
amekabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni 2 kutoka kwa taasisi za umma
kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea wilayani
Hanang mkoani Manyara.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Ikulu, Chamwino ambapo Rais Samia
amekabidhiwa hundi hiyo kutoka kwa Msajili wa Hazina, Bw. Nehemia Mchechu kwa
niaba ya taasisi mbalimbali za serikali.
Aidha, Rais Samia amesema lengo la kuwachangia waathirika hao ni kuweza
kuwapatia mahitaji muhimu ili waweze kurejea katika maisha yao ya kawaida.
Hali kadhalika, Rais Samia ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kukamilisha tathmini ya
maafa hayo kwa waathirika ili serikali ianze mchakato wa kuwarejesha katika makazi
rasmi.
Rais Samia amewataka Watanzania kutunza mazingira kwa kusafisha na kuacha
kutupa takataka katika mitaro na kuhakikisha inazibuliwa kwa wakati ili mvua
zinaponyesha iweze kutiririsha maji.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amezishukuru taasisi za umma,
wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla kwa kuonesha mshikamano katika
kusaidia waathirika wa maafa hayo.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi za Umma
wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na
Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu


0 Reviews