RAIS MWINYI NA MTOTO WA AMIRI WA QATAR

RAIS MWINYI NA MTOTO WA AMIRI WA QATAR

Size
Price:

Read more

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.
Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na mtoto wa Amiri wa zamani
wa Qatar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Makumbusho ya Taifa
Mhe. Sheikha Al Mayassa bint Hamad bin Khalifa Al Thani katika
hoteli ya Sheraton ambapo ndipo linapofanyika Jukwaa la Doha
(Doha Forum).
Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Mhe. Sheikha Al Mayassa kwa
niaba ya Serikali ya Qatar kupitia mradi wa miaka mitatu wa “Out
Of School Children” (OOSC) uliofadhiliwa na Qatar Fund for
Development ambao umetekelezwa kwa kushirikiana na Shirika
la Umoja wa Mataifa UNICEF pamoja na Education Above All
Foundation (EAA).
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema mradi huo umefanikiwa kwa
kiasi kikubwa baada ya kuwarudisha shuleni watoto zaidi ya
35,500 Unguja na Pemba na kuendelea na masomo.
Rais Dk. Mwinyi pia amependekeza kwa Mhe. Sheikha mpango
wa kubadilishana wanafunzi katika fani ya Ukutubi kutoka

Zanzibar kuja kujifunza na kubadilishana uzoefu na maarifa katika
Maktaba ya Doha.
Kabla ya kumaliza mkutano huo, Rais Dk. Mwinyi amemweleza
Mhe. Sheikha kuwa Zanzibar ina utajiri wa Mambo ya Kale hivyo
kutokana na uzoefu mzuri wa Qatar katika masuala hayo,
ingekuwa ni fursa nzuri kusaini Mkataba wa Makubaliano (MOU).
Hii itawawezesha wataalamu kutoka Qatar kubadilishana uzoefu.

0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *