Read more
Wakati huo huo Rais Dk. Mwinyi alizungumza na Naibu Mkurugenzi Mkuu
anashughulikia kurugenzi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, (EU) Martin Seychell,
aliefika Ikulu kwa mazungumzo.
Katika masungumzo yao pia waligusia masuala mbalimbali ya elimu na sekta
nyengine za maendeleo ikiwemo huduma za afya na usalama wa chakula.
Rais Dk. Mwinyi, aliishukuru (EU) kupitia Shirika la Kimataifa la “Global
Partnership for Education” (GPE) kwa msaada wanaoutoa kwa Tanzania ikiwemo
Zanzibar kwenye mfumo mzima wa sekta ya Elimu Zanzibar, kwa ngazi zote
kutoka msingi, sekondari hadi vyuo vikuu.
Dk. Mwinyi alieleza licha ya changamoto za Elimu zilizopo, Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar imejitahidi kuzipatia suluhisho la kudumu kwa msaada wa EU na
GPE, ikiwemo kuongeza madarasa mengi yaliyopunguza msongamano wa idadi
kubwa ya wanafunzi madarasani kwa wakati mmoja pamoja na kuongeza walimu,
kuboresha na kuongeza nyenzo za kufundishia, kuweka miundombinu ya kisasa
inayoendana na teknolojia iliopo pamoja na kuimarisha mazingira bora ya skuli za
Serikali.
Naye, Bw. Martin Seychell aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
juhudi ilizozichukua kuimarisha sekta ya elimu kwa ngazi zote na kueleza, elimu
ndio mustakbali bora wa mageuzi ya uchumi na maendeleo ya dunia.
Alisema, kati ya fursa na misaada mingi inayotolewa na EU kupitia shirika la GPE,
Zanzibar ni moja kati ya zaidi ya mataifa 30 yanayoendelea duniani, kunufaika na
fursa za elimu ikiwemo kutoa mafunzo ya teknolojia kwa walimu wa ngazi za vyuo
pamoja na sekondani kwa wasichana.
GPE ni Shirika la Kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya (EU) linalotoa ufadhili wa
elimu kwa wadau mbalimbali kwa lengo la kuimarisha mifumo bora ya elimu kwa
nchi zinazoendelea ili kuongeza kasi ya idadi ya watoto wanaokwenda skuli
kusoma. Shirika hilo pia huyaweka pamoja mataifa yanayoendelea, wafadhili,
mashirika ya kimataifa, mashirika ya kiraia, mashirika ya walimu, sekta binafsi na
Umma.


0 Reviews