SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imejikita kuleta mageuzi
makubwa kwenye sekta zote za maendeleo pamoja na kuwajengea uwezo
watu wake ili kuongeza kasi ya uchumi nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi,
ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Rais wa Taasisi ya Ufadhili
wa masomo nchini Uturuki (YTB) kutoka Wizara ya Utamaduni na Utalii
inayoshughulikia Mambo ya Nje, Bw. Abdullah Eren na ujumbe wake waliofika
kumtembelea.
Alisema, Serikali imepiga hatua kubwa kuimarisha miundombinu ya kisasa kwa
sekta zote za uchumi na jamii ikiwemo kuboresha ujenzi wa barabara, sekta za
elimu, afya na uwekezaji.
Dk. Mwinyi alisema, Uturuki imekua na ushirikiano wa katibu na Tanzania kupitia
ubalozi wake uliopo nchini kwa kuungamkono na kutekeleza miradi mbalimbali ya
Serikali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, ujenzi wa Uwanja wa
Amani na miradi mengine ya jamii, elimu, afya na ujenzi wa nyumba za maakazi
kwa wanchi wa Zanzibar kupitia kampuni ya “Orkun” kutoka Uturuki.
Aidha, ameishukuru Serikali ya Uturuki kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali za
SMT na SMZ hasa kuungamkono juhudi mbalimbali za maendeleo.
Rais, Dk. Mwinyi pia, aliipongeza Uturuki kwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania
ikiwemo Zanzibar, hasa kutoa fursa nyingi za ufadhili wa masomo ya elimu ya juu
kwa fani mbalimbali ambapo Watanzania wengi wako nchini Uturuki wakiendelea
na mafunzo ya muda mfupi na mrefu.
Alisema, ufadhili ni moja ya msaada mkubwa unaotolewa na Serikali ya Uturuki
kwa Tanzania kwenye kukuza ushirikiano mwema uliopo baina ya mataifa mawili
hayo.
Pia, Dk. Mwinyi aliisifu Uturuki kwa kuwa na wawekezaji wengi Tanzania pamoja
na kampuni mbalimbali zinazoendendesha shughuli zao nchini.
Alisema kampuni hizo zimekua na ushirikiano mzuri na Seriikali za Tanzania
katika kuungamkono na kusaidia kwenye miradi ya maendeleo.
Naye, Bw. Abdullah Eren alimueleza Rais Dk. Mwinyi bado Serikali yao
inaendelea kutoa ufadhili wa masomo kwa Tanzania hususan, Zanzibar.
Amesema, Serikali ya Uturiki inatarajia kutoa ufadhili mkubwa wa masomo kwa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar kupitia vyuo vya amali vilivyopo
nchini na kumueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba tayari wamefanya mazungumzo na
Waziri wa Elimu, Lela Muhamed Mussa kujadili suala hilo.
Bw. Aliwapongeza Wazanzibari kwa kuzikimbilia fursa nyingi zinazotolewa na
Serikali ya Uturuki na kueleza kuwa asilimia kubwa ya Wazanzibar wako Uturuki
kwa masomo na fursa nyengine za maendeleo.
Alisema, ujasiri wa Watanzania nchini Uturuki unatokana na ushirikiano na
uhisiano mzuri wa Dipolomasia uliopo baina ya pande mbili za ushirikiano.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi wa Uturuki nchini Tanzanzia, Dk. Mehmet
Gulluoglu, alimuomba rais Dk. Mwinyi kuangalia uwezekano wa kuipatia fursa
Serikali ya Uturi kuanzisha makumbusho ya kidijitali itakayohusisha masuala ya
historia na utamaduni ili kuvutia zaidi watalii watakaoingia nchini.
Aidha, alieleza fursa hiyo pia itachochoa kasi ya ongezeko la watalii na fursa
nyingi za uwekezaji na biashara nchini.