RAIS SAMIA: SERIKALI ITAREJESHA HUDUMA ZOTE ZA MSINGI ZA KIJAMII

RAIS SAMIA: SERIKALI ITAREJESHA HUDUMA ZOTE ZA MSINGI ZA KIJAMII

Size
Price:

Read more

 




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia

wakazi wa mji mdogo wa Katesh walioathirika na mafuriko makubwa kuwa serikali itarejesha

huduma zote za msingi za kijamii.

Rais Samia amesisitiza kuwa serikali itaendelea kufanya tathmini ya uharibifu wa mali huku

akiiagiza Wizara ya Nishati kuangalia uwezekano wa upatikanaji wa umeme wa dharura

baada ya miundombinu kuharibika na maafa haya ili shughuli za uopoaji zifanyike usiku na

mchana.

Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi na waathirika mara baada

ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na mafuriko hayo na kushuhudia hali halisi ya uharibifu

wa maafa.

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa mbali na michango mbalimbali iliyotolewa ndani ya nchi

lakini pia kumetolewa takriban Shilingi bilioni 2.5 kutoka kwa wahisani walioshiriki kwenye

mkutano wa COP 28, Dubai.

Miongoni mwa maeneo aliyotembelea Rais Samia ni Hospitali ya Tumaini wilayani humo

kwa ajili ya kuwajulia hali na kuwafariji majeruhi na pia shule ya Sekondari ya Katesh

ambapo ndipo makazi ya muda yalipowekwa ili kuwastiri waathirika hao.

Vile vile, Rais Samia ametaka tahadhari zote za msingi zichukuliwe ili kusitokee janga

jingine la mlipuko wa magonjwa hivyo kuheshimu kanuni za usafi kwani amesema majanga

wakati mwengine huzua maradhi kama kipindupindu.

Hivyo Rais Samia ameielekeza Wizara ya Maji kuhakikisha huduma za maji safi na salama

zinaendelea kupatikana muda wote huu hususan maeneo yaliowekwa makambi ya kustiri

waathirika wa janga hilo.

Mafuriko mazito yaliotokea yamesababisha vifo vya Watanzania 76 hadi sasa, huku kaya

1,150 zikiwa zimeathirika na watu 5,600. Pia kumekuwa na majeruhi zaidi ya 117 pamoja na

uharibifu wa miundombinu ya barabara, maji na umeme.

0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *