Read more
NA HADIA KHAMIS, BOSS TV
BARAZA la Sanaa Tanzania ( BASATA) linakusudia kutoa vyeti maalum kama sehemu ya pongezi kwa wasanii wa kikundi cha sarakasi pamoja na wasanii wa bongo fleva kwa kutii Sheria namba 23 ya 1984 iliyofanyiwa marekebisho 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari Jana Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Basata Dk. Kedmon Mapana amesema kuwa Sheria hiyo inawataka wasanii kabla ya kutoka kwenda nje ya nchi ni lazima wapate kibali kutoka Basata.
"Basata ndio walezi wa wasanii wote hivyo ni lazima kila msaanii anaposafiri kwenda nchi za nje kwa ajili ya kufanya show ni lazima aje achukue kibali Basata ilu kujua taarifa za Msanii husika", amesema DK Mapana.
Amesema vikundi vilivyofanya vizuri katika kuomba ruhusa ni pamoja na Ramadhani brothers upande wa madj ni hamad Hassan Mberwa , Ali kiba na Diamond platinum.
Hata hivyo amewataka wasanii ambao hadi leo hawajahuisha taarifa zao wakahuishe taarifa hizo kabla ya Disemba 30 mwaka huu ili kuepuka kufutiwa taarifa zao.
Amesema Basata ina mpango wa kufutia usajili vikundi vyote vya sanaa, makampuni, mapromota ambao wanaendesha shughuli za sanaa bila kufuata kanuni na utaratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha amesema ni vyema nguvu kubwa ikawekezwa kwa wasanii wa kike katika suala zima la kuomba vibali kufanya show nje ya nchi.



0 Reviews