Read more
NA HADIA KHAMIS, BOSS TV
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema ulaji sahihi wa chakula mchanganyikosio gharama hivyo elimu iendelee kutolewa kwa jamii kuhusu matumizi sahihi ya chakula mchanganyiko Ili kutokomeza utapiamlo na magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Ushauri huo ameutoa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa kitaifa wa ulaji sahihi ulioandaliwa ili kuimarisha matumizi sahihi ya chakula mchanganyiko hapa nchini ulioandaliwa na TFNC kwa kushirikiana na fao.
Aidha amesema mwongozo huo umeandaliwa kwa kutumia taarifa na Takwimu za kisayansi zilizofanyika nchini na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 10 barani Afrika ambazo zinamuongozo kama huo.
“Nimefahamishwa kwamba mwongozo huu ulioandaliwa kwa kuhusishwa Wadau mbalimbali kutoka ngazi zote. Pia wananchi wa kawaida walipata fursa ya kutoa maoni yao kwenye jumbe na michoro mbalimbali iliyotumika kwenye mwongozo huu,” amesema Waziri Ummy na kuongeza,
“Tunapozindua mwongozo huu, tunatekeleza moja kwa moja maelekezo ya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kupanua wigo wa Utiaji taarifa za pushed kwa wananchi,”.
Waziri Ummy ametumia fursa hiyo kuwashukuru Wadau wote walioshirikiana na Serikali katika kutokomeza utapiamlo wa aina zote.
“Leo kwa kipekee kabisa ninawashukuru FAO na Umoja wa Ulaya kwa mchango wao mkubwa katika kuunga mkono juhudi zetu za kuboresha hali ya lishe kwa Watanzania na kwa kufadhili maandalizi ya mwongozo huu. Asanteni sana FAO na Umoja wa Ulaya,” ameshukuru Waziri Ummy.
Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewaelekeza Maafisa Lishe, Wataalam wa Afya, Watafiti, Wataalam wanaotoa elimu ya lishe katika jamii, walimu na wadau wote wanaojishughulisha na Utoaji elimu ya afya ya jamii na lishe kuhakikisha wananchi wanafikiwa na kuutumia vizuri mwongozo huo.
Kadhalika ameitaka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNwashirikiane na kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kuandaa jumbe fupi fupi zinazoweza kutumika katika vyombo mbalimbali vya habari kama vile Televisheni, Redio, Magazeti na Mitandao ya kijamii ili kufikisha ujumbe mahususi wa mwongozo huo.
Sambamba na hayo Waziri Ummy amebainisha kuwa atawasiliana na OR Utumishi ili waelekeze Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Mashirika ya Umma kutoa elimu ya lishe katika vikao vyote vinavyofanyika katika maeneo yao vinavyohusisha watu 50 au zaidi kama mkakati wa kurahisisha kukabiliana na uzito uliozidi na unene Serikalini.
Hata hivyo ametoa wito kwa viongozi hususan katika ngazi za Mikoa na Halmashauri kuhakikisha kuwa mwongozo huo unasambazwa Kwa njia rahisi ambayo wananchi wataielewa ili kufikia malengo ya mwongozi huo.



.jpeg)
0 Reviews