RAIS WA ROMANIA, DKT SAMIA KUJADILI SEKTA YA AFYA, KILIMO, NISHATI NA MADINI

RAIS WA ROMANIA, DKT SAMIA KUJADILI SEKTA YA AFYA, KILIMO, NISHATI NA MADINI

Size
Price:

Read more

 





RAIS wa Romania, Klaus Iohannis, amewasili nchini kwa ziara ya kitaifa kuanzia jana Novema 16 hadi 19, 2023 kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki.

Lengo la ziara hiyo ni pamoja na kushawishi uwekezaji zaidi na kuvutia watalii wengi kutoka nchini Romania.

Aidha katika mazungumzo rasmi yatakayofanyika tarehe 17 Novemba 2023 rais huyo na mwenyeji wake watajadili namna bora ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati sekta za elimu, afya, kilimo nishati na madini.

Kabla ya kuondoka nchini tarehe 19 Novemba 2023 Rais wa Romania atapata fursa ya kwenda Zanzibar ambapo atazungumza na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi na kutembelea mji mkongwe ambao ni moja kati ya vivutio vikubwa vya utalii duniani

0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *