Read more
MENEJA habari Simba SC, Ahmed Ally amesema mechi yao dhidi ya Asec Mimosa inatarajiwa kuchezwa November 25 mwaka huu katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam majira ya saa 10 jïoni.
Akizungumza na waandïshi wa habari leo Novemba 16, 2023 Ahmed Ally amesema kuwa waamuzi wa mchezo huo wanatokea nchi ya Misri na tiketi za mechi hiyo zimeanza kuuzwa kuanzia leo hii.
"Tiketi tunaanza kuuza leo, nunueni tiketi twendeni uwanjani. Ni kweli tulikuwa hatuchezi mpira wetu wa kuvutia lakini tunakwenda kubadilisha benchi la ufundi, tunategemea Simba itakayokuja itakuwa vizuri zaidi," anasema Ahmed.
Akizungumzia suala la tiketï amesema viingilio vitaanzia mzunguko 5,000,Vip B 20,000,Vip C 10,000, Vip A 30,000 na Platinumz ni 150,000.
Akizungumza suala la tuzo Ahmed amesema kuwa Tuzo ya Mashabiki Bora wa AFL 2023 haitakaa kwenye ofisi za Simba bali itakuwa inatembea kwenye matawi mbalimbali. Lakini pia tutakuwa na mfano ya tuzo kama hii ambayo tutaipeleka sehemu mbalimbali ili wabaki na kumbuumbu.
"Kuhusu mabango tumeyaona na tuna kitengo cha sheria, wanaangalia kuona kama inafaa kuchukua hatua au kuacha lakini hili tumesababisha sisi Simba. Wakati ujao wachezaji wafanye kila linalowezekana hiyo kadhia isitokee tena."
"Safari hii tunakwenda kuwashangaza watu, tutaujaza uwanja wa Mkapa. Niwambie Wanasimba kama una hasira uje nazo furaha utaikuta uwanjani. Kauli mbiu yetu ya mchezo dhidi ya ASEC Mimosas ni Twendeni Kinyama, Mashabiki Bomba."Ahmed Ally.


0 Reviews