Read more
Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) limemchagua Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, kuwa Rais wa Mkutano wa 153 wa Umoja huo unaofanyika jijini Arusha.
Uamuzi huo umefikiwa leo Oktoba 6, 2026, siku ya pili ya Mkutano wa 153 wa IPU unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), ambao unaendelea kuwakutanisha viongozi na wajumbe kutoka mabunge mbalimbali duniani. Mkutano huo umeanza kuanzia jana Oktoba 5 hadi 9, 2026.
Hoja ya kumchagua Zungu kuwa Rais wa Mkutano huo ilitolewa na Spika wa Bunge la Wawakilishi la Uingereza (House of Commons), Sir Lindsay Hoyle, na kuungwa mkono na baadhi ya nchi, ikiwemo Uganda na Umoja wa Falme za Kiarabu.

0 Reviews