Read more
Dar ea salaam - Tanzania imeendelea kujijengea heshima na kuaminika kimataifa kutokana na kasi ya maendeleo ya kiuchumi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamebainishwa na viongozi wa World Bank wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam kati ya Rais Samia na aliyekuwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Nathan Belete pamoja na mrithi wake, Firas Raad.
Katika uchambuzi wa kitaalamu wa mawasiliano ya serikali, kauli zilizotolewa na viongozi hao zinaonesha namna Tanzania ilivyoendelea kuaminika kama moja ya nchi zenye uchumi imara na mazingira bora ya maendeleo barani Afrika.
Rais Dkt. Samia akutana na Kuzungumza na aliyekuwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Nathan Belete ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Miradi ya Benki hiyo, Kanda ya Afrika, Ikulu Jijini Dar es Salaam
TANZANIA YAJENGA TASWIRA IMARA KIMATAIFA
Akizungumza kuhusu uzoefu wake wa kufanya kazi nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka minne, Nathan Belete amesema Tanzania ni nchi yenye watu wazuri, utulivu na mfumo mzuri wa usimamizi wa maendeleo, huku akieleza kuridhishwa na ushirikiano uliopo kati ya Serikali, wananchi na wadau wa maendeleo.
Belete ameipongeza Tanzania kwa mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, nishati, maji na usafi wa mazingira vijijini, akieleza kuwa hatua zilizofikiwa zinaonesha uwezo mkubwa wa Serikali katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi.
DIRA YA TAIFA 2050 YAPOKELEWA KWA MATUMAINI MAKUBWA
Benki
ya Dunia pia imeonesha matumaini makubwa kuhusu utekelezaji wa Dira ya
Taifa ya Maendeleo 2050 inayotarajiwa kuanza Julai mwaka 2026.
Kwa
mujibu wa Belete, Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kutumia nguvu ya
vijana pamoja na sekta binafsi kama msingi wa kuharakisha maendeleo ya
kiuchumi na kuongeza ajira.
Amesema
Benki ya Dunia inaiona Tanzania kama nchi yenye uwezo mkubwa wa kuvutia
uwekezaji wa sekta binafsi katika miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo
reli ya kisasa ya SGR, bandari pamoja na sekta ya nishati.
Kauli
hiyo inaonesha namna ambavyo ajenda ya maendeleo ya Serikali ya Awamu
ya Sita imeanza kuzaa matokeo chanya katika macho ya jumuiya ya
kimataifa.
MAGEUZI YA ELIMU, AFYA NA AJIRA ZA VIJANA YAPONGEZWA
Katika
mahojiano hayo, viongozi wa Benki ya Dunia wameeleza kuridhishwa na
hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha huduma za afya,
elimu na maendeleo ya vijana.
Belete
ametaja maboresho ya mitaala ya elimu pamoja na msukumo mkubwa
uliowekwa katika elimu ya ufundi na stadi kuwa sehemu muhimu ya
maandalizi ya vijana wa Tanzania kwa uchumi wa kisasa.
Kwa upande wake, Firas Raad
amesema ajenda ya ukuaji wa uchumi na ajira itaendelea kuwa eneo muhimu
la ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania.
Amesisitiza
kuwa ili kupunguza umaskini kwa ufanisi, kuna umuhimu wa kuendelea
kuwekeza katika elimu, afya, hifadhi ya jamii pamoja na miundombinu
muhimu kwa maendeleo ya wananchi.
TANZANIA YATAJWA KUWA MFANO WA UTEKELEZAJI WA MIRADI
Katika
sehemu nyingine ya mazungumzo hayo, Nathan Belete amesema Tanzania
imeonesha kuwa sekta ya umma inaweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa
pale panapokuwa na dhamira ya kisiasa, uratibu mzuri na usimamizi
madhubuti wa miradi ya maendeleo.
Ametaja
mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya nishati, maji vijijini pamoja
na huduma za usafi wa mazingira kuwa ushahidi wa uwezo wa Serikali
katika kuleta matokeo yenye manufaa kwa wananchi.
Kwa
tafsiri ya kitaalamu, kauli hiyo ni ishara ya kuendelea kuimarika kwa
mfumo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini chini ya Serikali ya
Rais Samia.
SEKTA BINAFSI YAPATIWA NAFASI MUHIMU
Benki ya Dunia pia imeweka mkazo katika umuhimu wa sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania.
Firas
Raad amesema kutokana na mahitaji makubwa ya maendeleo, kuna umuhimu wa
kuongeza ushiriki wa mitaji ya sekta binafsi ili kusaidia kugharamia
miradi mikubwa ambayo Serikali haiwezi kuitekeleza peke yake.
Amesema
Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika
kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji
zaidi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.
Kwa
ujumla, kauli za viongozi wa Benki ya Dunia zinaonesha wazi kuwa
Tanzania imeendelea kujenga imani kubwa kimataifa kutokana na utulivu wa
kisiasa, usimamizi mzuri wa uchumi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo
pamoja na maono ya muda mrefu ya maendeleo ya Taifa.
Katika
kipindi ambacho dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi,
Tanzania inaendelea kuonekana kama moja ya nchi zenye mustakabali mzuri
wa maendeleo barani Afrika, huku ajenda za maendeleo zinazotekelezwa na
Serikali ya Rais Samia zikipewa matumaini makubwa na wadau wa maendeleo
duniani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Nathan Belete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2026. Belete ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Miradi wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, alifika Ikulu kwa ajili ya kumuaga Rais Dkt. Samia mara baada ya kuhudumu katika nafasi yake ya awali kwa kipindi cha miaka minne. Pia aliambatana na mrithi wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo anayesimamia nchi za Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe Firas Raad.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na aliyekuwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Nathan Belete ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Miradi ya Benki hiyo, Kanda ya Afrika, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2026.





.jpeg)


0 Reviews