Read more
Na HADIA KHAMIS, BOSS TV
MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Abass Mtenvu amewataka wananchi wenye uwezo kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalumu katika suala zima la utoaji wa sadaka.
Ushauri huo ameutoa leo Machi 28 Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akiwakabidhi futari kikundi cha watu wenye ulemavu.
Mtenvu amesema kuwa watu wengi wanasahau kundi la watu wenye mahitaji maalumu ili hali ndio kundi kubwa linalohitaji msaada wa futari.
"Hawa ni marafiki zangu nimekuwa nikiwapa sadaka kila mwaka na kwa sababu ni kundi ambalo linasahaulika ndio maana nawapa kipaombele ni vyema wengine nao wawasaidie wenye uhitaji", amesema Mtenvu.
Akizungumza Mara bada ya kupokea futari hiyo Ashura Mwinyimvua amesema imekuwa ni kawaida kila mwaka kwa kiongozi huyo kuwakumbuka kundi la watu wenye uhitaji maalum jambo linalowazidishia mapenzi baina yao na kiongozi huyo.
"Jambo la kushukuru Mtenvu ni rafiki yetu, ni mlezi wetu na ndio maana mpaka sasa huu ni mwaka wa 10 anatukumbuka na ndio maana tupo pamoja naye", amesema Ashura.
Amesema ni vyema kwa watu wengine kuiga mfano huo wa kusaidia wenye uhitaji na Mungu atawaongezea wanapopunguza.
Miongoni mwa vitu vilivyotolea
kama sadaka na kiongozi huyo ni pamoja na unga wa ngano, mafuta ya kupikia, maji
na mchele.



0 Reviews