MOI WAANZISHA HUDUMA YA UPASUAJI WA MISHIPA YA MGONGO KWA NJIA YA MATUNDU

MOI WAANZISHA HUDUMA YA UPASUAJI WA MISHIPA YA MGONGO KWA NJIA YA MATUNDU

Size
Price:

Read more

Na HADIA KHAMIS, BOSS TV

TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo MOI kwa mara ya kwanza imeanzisha huduma ya upasuaji wa mishipa ya mgongo kwa njia ya matundu (Endoscopic Neurospine Surgery).

Huduma hiyo imeanzishwa kufuatia Kongamano la Kimataifa la Madaktari Bingwa wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (Global Neurosurgery course) ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya MOI na Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha Marekani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI Prof. Abel Makubi amesema tayari wagonjwa 13 wa mgongo wamefanyiwa upasuaji kwa mafanikio makubwa katika siku mbili Jumatano na Alhamisi toka kuanza kwa huduma hiyo.

Amesema jumla ya madaktari bingwa 120 wanashiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Amesema uanzishwaji wa huduma hiyo inayotumia teknolojia ya kisasa itasaidia kuwapunguzia wananchi gharama za kufuata matibabu ya aina hiyo nje ya nchi na kukuza tiba utalii hapa nchini.

“Hii ni kwa mara ya kwanza kwa MOI na ni mara ya kwanza kwa Taifa kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia matundu (Endoscopic Spine Surgery), kwa dhati tunakishukuru chuo kikuu cha Weill Cornel cha Marekani kwa ushirikiano huu muhimu na kwa niaba ya menejimenti naahidi tutauenzi” amesema Prof. Makubi 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upasuaji wa Mgongo kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornel Marekani Profesa Roger Hartl ameahidi kuendeleza ushirikiano na Taasisi ya MOI katika kuendelea kuwajengea uwezo wataalamu kuwezesha tafiti za kisayansi na vifaa tiba vya upasuaji ili iweze kuwa kituo mahiri cha upasaji wa mgongo barani Afrika.

“Lengo letu kuiona MOI ikiwa kituo cha umahiri kwenye kutoa tiba na mafunzo kwa mataifa mengine juu ya upasuaji wa mgongo kwa kutumia matundu, nimefurahi kuona namna ambavyo MOI inathamini ushirikiano wetu na ninaahidi kuuendeleza” amesema Profesa Hartl.

0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *