WATU 70 WADAKWA KWA TUHUMA MBALIMBALI ZANZIBAR

WATU 70 WADAKWA KWA TUHUMA MBALIMBALI ZANZIBAR

Size
Price:

Read more

 


Katika kukabilianana na kero wanazofanyiwa watalii katika fukwe mbali mbali,

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Wakaskazini Unguja imefanya operesheni

maalum na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa sabiini kwa makosa mbalimbali.

Akizungumza na Waandishi wahabari huko Ofisini kwake Mkototoni, Mkuu wa

Mkoa wa Kaskazini Unguja ambaae ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na

Usalama wa Mkoa huo Mheshimiwa RASHID HADID RASHID amesema

Operesheni hiyo ni maagizo ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza

la Mapinduzi DK. HUSSEN ALI MWINYI ya kuwataka Wakuu wa Mikoa

kuweka Mazingira salama kwa wanachi na watalii katika maeneo yao.

Kwaupande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kamishna

Msaidizi wa Polisi DANIEL SHILA ameeleza kuwa miongoni mwa waliokamatwa

katika Opersheni hiyo ni TWALIB SHAABAN AZUBERI (39) raia wa Kenya

ambae amekamatwa na dawa za kulevya.

Aidha amesema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Vikosi vya Ulinzi na

Usalama katika Operesheni hizo ili kuhakikisha Mkoa huo unaendelea kuwa

Salama kwa wananchi na kuendelea kuvutia watalii.

0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *