Read more
RAIS DK.MWINYI AMESHIRIKI CHAKULA CHA USIKU NA GPE IKULU
ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali
Mwinyi amejumuika pamoja na Uongozi wa bodi ya Wakurugenzi wa
Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) ukiongozwa na Mwenyekiti
wake Dkt.Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika chakula cha usiku alichowaandaliwa Ikulu Zanzibar tarehe
04 Disemba 2023.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE Laura
Frigenti pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini na Vyombo vya
ulinzi na usalama.
Aidha Vikao vya GPE vitafanyika Zanzibar na kufunguliwa kesho tarehe 05
hadi 06 Disemba ikiwa ni mara ya kwanza kwa shirika hilo la kimataifa
kufanya vikao vyake vya bodi barani Afrika.
Vilevile Shirika hilo limeisaidia Zanzibar katika sekta ya elimu fedha za
kigeni dola za kimarekani Milioni 11.7 kwa ajili ya kusaidia elimu ya msingi
ikiwemo miradi itakayoanza Januari 2024 kwa kujumuisha mafunzo ya
walimu, utendaji, usimamizi wa elimu , masuala ya jinsia na mjumuisho.
Kwa mujibu wa Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza
GPE, shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya Dola za
Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia
sekta ya elimu bara na Zanzibar.


0 Reviews