ZIFAHAMU AINA KUU MBILI ZA KISUKALI


DAKTARI kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma Dkt. Alemiana Alex
 amesema kutokufanya mazoezi, unene uliopitiliza, kula vyakula vya wanga na mafuta kwa wingi, kunywa pombe kupita kiasi  vinaweza kusababisha ugonjwa wa Kisukari.

Hayo yamebainishwa Novemba 14, 2023 na Daktari kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma Dkt. Alemiana Alex  ambapo amesema mambo ya kuzingatia katika kuepuka ugonjwa wa Kisukari ni pamoja na kuepuka kunywa pombe kupita kiasi, kupunguza matumizi ya sukari kwa wingi.

Unachotakiwa kufanya ni kula mbogamboga kwa wingi, kufanya mazoezi pamoja na kupunguza msongo wa mawazo na kuwa na desturi ya kupima afya mara kwa mara.


BOSS TV

Hii ni Official blog ya BOSS MEDIA kwa habari za siasa, jamii, elimu, burudani na michezo tufuatilie kwa uhakika zaidi

Post a Comment

Previous Post Next Post