TANESCO KUJENGA KITUO KIDOGO CHA UMEME  USHETU

TANESCO KUJENGA KITUO KIDOGO CHA UMEME USHETU

Size
Price:

Read more

SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) lina mpango wa kujenga kituo kidogo cha umeme (Switching Station) kwenye Wilaya ya Ushetu eneo la Nyamirangano ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme wilayani humo. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa  Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati akijibu swali la Mbunge wa Ushetu Emanuel Peter Cherehani aliyetaka kujua je nini mkakati wa Serikali wa kupeleka umeme wa uhakika   katika halmashauri za Ushetu, Msalala, na Kahama. 

Aidha, Kapinga amesema sambamba na hilo TANESCO pia itaongeza njia nyingine za umeme kutokea kituo hicho kwenda Ushetu, Msalala,  Msalala, na Kahama. 

Amesema, ujenzi wa mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 12 na  mradi unategemewa kukamilika Mwaka wa Fedha 2024/2025.

0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *