Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay wafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi

Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay wafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi

Size
Price:

Read more

 


Ajira, ujuzi wa ufundi na kuimarika kwa biashara ndogo ni miongoni mwa manufaa ambayo wananchi wameanza kupata kutokana na ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay, wilayani Nyasa, Mkoa wa Ruvuma, ambao umefikia asilimia 78.


Baadhi ya vijana wanaoshiriki katika ujenzi huo wamesema wamepata kipato kinachowawezesha kuhudumia familia zao, huku wengine wakipata fursa ya kujifunza stadi za ufundi zitakazowawezesha kujiajiri baada ya mradi kukamilika.


Vijana hao walieleza manufaa hayo walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kuimarisha usafirishaji wa mizigo na biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za Malawi, Msumbiji na Zambia.


Mhandisi Msimamizi wa Mradi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), John Paul, amesema eneo la Mbamba Bay lilichaguliwa baada ya upembuzi yakinifu uliofanyika mwaka 2023 kubaini umuhimu wake katika kuimarisha huduma za bandari.


Amesema utekelezaji wa mradi unaendelea vizuri kutokana na usaidizi wa Serikali na upatikanaji wa fedha zinazomwezesha mkandarasi kulipwa kwa wakati.


“Tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na kutoa fedha kwa wakati,” amesema Paul.


Pia, amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, kwa kusimamia utekelezaji wa mradi huo ili kufanikisha malengo yaliyowekwa na Serikali na kuchochea ukuaji wa Bandari ya Mbamba Bay pamoja na bandari nyingine nchini.


Kwa upande wake, Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Anova, Agathon Mwenda, amesema kazi za ujenzi zinaendelea vizuri na kwamba kampuni hiyo inalenga kukamilisha mradi ifikapo Februari 26, 2027, kama ilivyoainishwa katika mkataba.

0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *