Read more
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Wakili Peter Daniel Madeleka kwa tuhuma za kudharau amri za Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, Wakili Madeleka alikamatwa Agosti 14, 2026, saa 9:30 alasiri katika eneo la Mikocheni B, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kukamatwa kwake kumetokana na tuhuma za kudharau amri za Mahakama Kuu zilizotolewa Julai 27 na Agosti 13, 2026.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, Wakili Madeleka anatarajiwa kufikishwa mahakamani Agosti 17, 2026 kwa hatua zaidi za kisheria.

0 Reviews