Read more
Zanzibar: MWINDAJI na Tik Toker maarufu kutoka jamii ya Wahadzabe, Chaba, ameeleza masikitiko yake kuhusu baadhi ya watu wanaotumia jina, picha na video zake kwenye mitandao ya kijamii bila kumhusisha wala kumpatia manufaa yoyote.
Akizungumza wakati wa Tamasha la Kimataifa la
Filamu Zanzibar, ZIFF 2026, Chaba alisema amekuwa akiona maudhui mengi
yanayosambazwa mtandaoni yakimhusisha yeye na maisha ya jamii ya Wahadzabe,
lakini mara nyingi wahusika wanaonufaika na maudhui hayo si watu wa jamii yake.
Chaba alisema umaarufu wake umechangia kuitangaza
jamii ya Wahadzabe duniani, lakini bado kuna changamoto ya watu kutumia picha
na video zake kwa ajili ya kujitengenezea kipato bila kupata kibali au
kushirikisha jamii husika katika faida zinazotokana na maudhui hayo.
Kauli yake imeibua mjadala miongoni mwa washiriki
wa ZIFF 2026 kuhusu haki za maudhui ya kidijitali, utamaduni na namna jamii za
asili zinavyoweza kunufaika na umaarufu unaotokana na matumizi ya mitandao ya
kijamii.
Chaba, ambaye amepata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kupitia video zinazoonesha maisha na utamaduni wa Wahadzabe, amekuwa mmoja wa sura zinazotambulika zaidi katika kuitangaza Tanzania kupitia urithi wa utamaduni wa asili.
0 Reviews