Baraza la Vyama vya Siasa lahimiza mazungumzo yenye staha kulinda amani ya taifa

Baraza la Vyama vya Siasa lahimiza mazungumzo yenye staha kulinda amani ya taifa

Size
Price:

Read more


BARAZA la Vyama vya Siasa nchini limeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kufungua nafasi ya majadiliano na mashauriano kati ya wadau wa kisiasa, hatua iliyotajwa kusaidia kulinda umoja, amani na mshikamano wa taifa.

 Akitoa taarifa ya maazimio ya kikao cha siku tatu cha baraza hilo kilichomalizika Juni 18, 2026 mjini Morogoro, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Ali Khatib alisema wajumbe wamekubaliana kuendelea kuhimiza mazungumzo yenye staha na kuepuka kauli zinazoweza kuleta mgawanyiko nchini.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe kutoka vyama 18 kati ya 19 vyenye usajili kamili, wakiwemo wenyeviti wa vyama, makatibu wakuu, viongozi wa wanawake na wajumbe wengin

wakati huo huo Watanzania Watakiwa Kutozingatia Taarifa Zisizo Sahihi za Mitandao ya Kijamii Kuhusu Ubia wa Tanzania na EU

Serikali imewataka wananchi kuachana na taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari ambazo zinapotosha ukweli kuhusu kura iliyopigwa na Bunge la Ulaya. 

Kupitia taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, imesisitizwa kuwa kura hiyo iliyopigwa Juni 18, 2026, kuhusu Mpango wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) kwa mwaka 2026 si uamuzi wa mwisho wa EU kuhusu programu hiyo yenye thamani ya Euro milioni 156. 

Serikali imebainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu tu ya mchakato wa ndani wa taasisi za EU ambapo Bunge limetoa maoni na mapendekezo kwa mamlaka nyingine zinazohusika na maamuzi ya mw…


0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *