RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Majaji tisa wa
Mahakama Kuu kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bw. Bakari Machumu, leo tarehe 20 Mei, 2026,
imesema kuwa wateule hao wataapishwa tarehe itakayotangazwa baadaye.
Walioteuliwa ni Majaji saba wa
Mahakama Kuu ya Tanzania na wengine wawili kutoka Mahkama Kuu ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa ni Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Abdi Shaaban Kagomba na
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Arusha, Mhe. Yohane Bokobora
Masara.
Wengine ni Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Bukoba, Mhe. Immaculata Kajetan Banzi
na Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar, Mhe. Rabia Hussein Mohamed.
Wateule wengine ni Jaji Mfawidhi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam, Mhe. Cyprian
Phocas Mkeha na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi,
Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina.
Wengine ni Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, Mhe. Iman, Daud Aboud, Jaji wa Mahkama Kuu ya
Zanzibar, Mhe. Mzee Ibrahim Ibrahim na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Masjala Ndogo Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Laurent Masabo.
0 Reviews