VYAMA VYA SIASA 12 VYAPONGEZA RIPOTI YA TUME YA JAJI CHANDE


DAR ES SALAAM: VIONGOZI mbalimbali wa vyama vya siasa zaidi ya 12 wameipongeza ripoti ya tume ya kuchunguza matukio ya tarehe 29 na baada ya uchaguzi iliyowasilishwa na jaji Chande na kuomba wale wote waliohusika na vurugu hizo kuchukuliwa hatua KALI za kisheria.

Katika mkutano huo uliofanyika hivi karibuni, viongozi hao pia waliipongeza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubaliana na mapendekezo yote yaliyopendekezwa na tume hiyo.

Katika mkutano huo, aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha NLD,  Doyo Hassan Doyo amesema Tume ya Jaji Chande iliyotumwa kufanya uchunguzi wa  Matukio ya Vurugu wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 imefanya kazi nzuri na inastahili pongezi kubwa.

"WITO wangu naomba wale wote waliosababusha au waliotoa viashairia vya ghasia hizo wachukuliwe hatua kali za kisheria Ili iwe fundisho daima," alisema Doyo.

viongozi wapo katika mkutano

Katika hatua nyingine vyama 12 vya siasa nchini vimeipongeza ripoti ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2026 vikisema kuwa ina uwezo wa kuliponya taifa.

Akizungumza Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha DP, Abdul Mluya, amesema maridhiano na mwafaka wa kuunganisha taifa unapaswa kufanywa na Watanzania wenyewe bila kuhusisha watu wa nje.

Vyama vilivyoshiriki mkutano huo ni, UDP, NRA, TLP, UMD, MAKINI, CCK, SAU, ADA TADEA, AAFP, NLD na DP.

Pia vimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka wazi ripoti hiyo, wakisema imeeleza ukweli wote bila kuficha jambo lolote, kwa lengo la kuponya vidonda vya taifa.

"Matukio yaliyotokea hayamhusu Rais pekee bali yanawahusu wadau wote wa kisiasa, hivyo hapaswi kujiona yuko peke yake," Mluya amesema.


Vyama hivyo vimedai kuwa matukio hayo hayakuwa maandamano bali yalikuwa mapinduzi, na kusisitiza kuwa kila Mtanzania ana wajibu wa kulinda amani ya nchi.

BOSS TV

Hii ni Official blog ya BOSS MEDIA kwa habari za siasa, jamii, elimu, burudani na michezo tufuatilie kwa uhakika zaidi

Post a Comment

Previous Post Next Post