SIRI YAFICHUKA: Ushirikiano wa wachochea vurugu na vyombo vya habari vya Kimataifa

SIRI YAFICHUKA: Ushirikiano wa wachochea vurugu na vyombo vya habari vya Kimataifa

Size
Price:

Read more


PICHA zinazoonesha  ushirikiano wa karibu kati ya  wachochezi wa vurugu za Oktoba 29 na shirika kubwa la kimataifa la habari, CNN zimeendelea kuvuja huku watumiaji wa mitandao wakielezea ushirikiano huo haramu ukiwa ni sehemu ya "mradi" mpana unaolenga kuchafua taswira ya Tanzania na kuhamasisha vurugu ili kufikia lengo la kuangusha Serikali iliyopo madarakani.

Miongoni mwa picha hizo ni hii inayomuonesha Maria Sarungi akizungumza na mwandishi wa CNN, Mwandishi Larry Madowo raia wa Kenya ambaye aliandika makala yenye uongo mkubwa ikiwamo kuwapo kwa kaburi la jumla pale kwa Kondo akidai ni picha za setelaiti. 

Hata hivyo, wanamtandao wanahoji kwa nini wao hawajaenda kuonesha makaburi hayo yanayotajwa na Satellite "fake" ya CNN.

Mwandishi huyo wa CNN alijaribu kutumia ushawishi wake kuaminisha umma kwamba shirika hilo lilikuwa na picha za satelaiti zinazothibitisha uwepo wa makaburi hayo.


0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *