SERIKALI YATOA KAULI BEI YA SIANIDI KUPANDA MIGODINI

SERIKALI YATOA KAULI BEI YA SIANIDI KUPANDA MIGODINI

Size
Price:

Read more


GEITA: CHAMA cha Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Geita (GEREMA) kimelalamikia uwepo wa changamoto ya kupanda kwa kemikali ya Sianidi inayotumika maalum kwa shughuli za uchechuaji wa madini ya dhahabu

Katibu wa GEREMA, Misana Nyabange amesema bei ya kemikali ya sianidi kutoka laki tano hadi milioni moja.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema serikali itafanya kikao maalum cha tathimini kesho Desemba 2, 2025 ili  kujadili kupanda kwa tatizo hilo.


Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ametoa kauli hiyo akiwa wilayani Nyang’hwale mkoani Geita katika hafla ya ugawaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo iliyofanyika Kijiji cha Nyijundu.

Katika kikao hicho wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Madini pamoja na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali watakuwepo.

Matumizi ya kemikali ya sianidi ni teknolojia za kisasa za uchenjuaji madini ya dhahabu yenye ufanisi wa kati ya asilimia 90-98 tofauti na asilimia 40-48 ya madini ya zebaki.

 

0 Reviews

Contact form

Name

Email *

Message *