Read more
DAR ES SALAAM: MREMBO wa mitandaoni na mfanyabiashara Jenifer Jovin, maafufu Niffer ameachiwa huru baada ya kufutiwa mashitaka ya uhaini.
Pia katika hilo aliyelkuwa mshitakiwa mwingine katika sakata hilo pamoja na Niffer ni Mika Chavala, ambaye pia ameachiwa huru kwa kufutiwa mashitaka ya uhaini.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ndiye aliyefuta mashitaka hauo na kuwaacha huru Niffer na Mika leo Jumatano, Desemba 3, 2025, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamuya.
Wakili wa Serikali Titus Aron aliwasilisha mashitraka hayo kwamba DPP hana tena nia ya kuendelea na mashitaka dhidi ya watuhumiwa hao ndipo Hakimu Lyamuya akatangaza kuwa mashtaka yote dhidi ya Jenifer na Mika yamefutwa, jambo lililozua shangwe, vifijo na nderemo kutoka kwa ndugu, marafiki na wananchi waliofurika mahakamani hapo.



0 Reviews