Read more
Na HADIA KHAMIS, DAR
WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye Jana amezindua mtandao wa bure utakaokuwa ukipatikana katika Uwanja wa Benjamin Makapa hapa jijini Dar es salaam.
Mtandao huo unaotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ni sehemu ya zawadi ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa wanamichezo waliojitokeza kushuhudia michezo katika uwanja huo huku mchezo wa Simba na Yanga ukiwa wakwanza katika uzinduzi huo.
"Ametuagiza tuhakikishe viwanja vyote vinakuwa na huduma hii ya mtandao wa bure kupitia shirikaletu la TTCL tumeanza na Uwanja wa Benjamin Mkapa na viwanja vingine vitafuata leo tunaanza na mchezo huu wa watani wa jadi.
"Na itakuwa ni sehemu ya zawadi ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa wapenda michezo wote ili mfurahie mpira huku mkituma picha zenu na hata picha za kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan," alieleza Nape.
Alisema watu wote walioko uwanjani wanaweza kuchati na kutuma picha huku wakiendelea kufurahia burudani ya mpira.


0 Reviews